Hizi-Ndizo-Teknolojia-5-Za-Kushangaza-Kutoka-DARPA
Defence Advanced Research Project Agency au kifupi DARPA ni shirika la serikali ya Marekani ambalo kazi yake kubwa ni kutengeneza teknolojia za ajabu kwa ajili ya usalama wa taifa la Marekani na kuendelea kuweka Marekani kama kinara wa teknolojia za hali ya juu kuliko nchi yoyote ile Duniani.
Kuna baadhi ya teknolojia ambazo hata wewe unazitumia pasipo kufahamu zimetengenezwa na shirika hilo la DARPA, kwa mfano, intaneti ni moja kati ya teknolojia ambazo ziligunduliwa na shirika hilo, na kwa mara ya kwanza intaneti ilikuwa inatumika kwa ajili ya jeshi la Marekani kabla haijaachiwa na kuanza kutumika katika jamii, ambapo teknolojia hiyo imeweza kuleta mapinduzi makubwa sana katika ulimwengu wa leo hii.
Zipo teknolojia nyingi sana ambazo zimegunduliwa na DARPA, kama tukisema tuanze uziorodhesha hapa tovuti yetu itajaa jamani. Hivyo leo tutaziangalia zile tano ambazo ni nzuri sana.
Warrior Web
Warrior-Web
Wanajeshi kwa kawaida wanatakiwa kubeba mizigo mizito ikiwamo silaa, na vifaa vingine wanapoenda mzigoni kwa kuliona hilo DARPA wakaamua kutengeneza roboti inayoitwa Warrior Web, roboti hiyo nyepesi inamkinga mwanajeshi dhidi ya maumivu ya kwenye magoti, mapaja na mabega pale anapokuwa amebeba mizigo yake mizito.
Nyumba zinazojirekebisha zenyewe
Nyumba-zinazojirekebisha-zenyewe
Mwaka 2016, DARPA walianzisha mradi unaoitwa Engineering Living Material, mradi huo ambao lengo lake kubwa lilikuwa ni kutengeneza nyezo za ujenzi ambazo zinaweza kujirekebisha pindi jengo au nyumba itakapoharibika katika hali yoyote ile.
ACTUV
ACTUV-au-ASW-Continous-Trail-Unmanned-Vessel
ACTUV au ASW Continous Trail Unmanned Vessel ni chombo ambacho kitakuwa na muonekano kama nyambizi ila kazi yake kubwa ni kusaka nyambizi za maadui, pasipo kuwa na mtu anayekiendesha ndani. Chombo hicho kitatumia teknolojia ya kuhisi vitu vingine chini ya maji ya hali ya juu, pia kitaweza kuendeshwa na watu ambao watakuwa nchi kavu.
XS-1 ndege ya masafa ya juu
XS-1-ndege-ya-masafa-ya-juu
Huku kampuni kama Space X wakifanikiwa kutengeneza ndege za angani ambazo zinaweza tumika kwa zaidi ya mara moja, DARPA nao wanatengeneza ndege ambazo licha ya kutumika kwa safari nyingi pia zitakuwa na uwezo wa kubeba mizigo yenye uzito wa kilo 1000 kwenda huko nje ya Dunia.
Teknolojia ya kuunganisha ubongo na kompyuta
Teknolojia-ya-kuunganisha-ubongo-na-kompyuta
Teknolojia hii ilitangazwa mwaka 2013, ambapo DARPA kushirikiana na vyuo vikuu, kampuni kubwa za teknolojia, wanasayansi wa ubongo, pamoja na mashirika mbali mbali nchini Marekani wataweza kutengeneza teknolojia ambayo itawezesha ubongo wa binadamu kuunganishwa na kompyuta hivyo kuweza kupakia na kupakuwa taarifa kutoka kwenye ubongo wa binadamu kwa urahisi zaidi.